December 6, 2020

 




KATIKA Uwanja wa Mkapa kuanzia saa 1:00 usiku leo Jumapili, kuna mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya Yanga na Ruvu Shooting ambapo mechi hiyo kuna rekodi inasakwa.

 

Ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 31, Yanga inakutana na Ruvu Shooting yenye pointi 23 zote zimecheza mechi 13.
Tangu msimu wa 2010/11,timu hizo zimekutana mara 18, Yanga imeshinda 13 na Ruvu Shooting ikishinda moja, huku
zikipatikana sare nne.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, alisema kuwa kila kitu kipo sawa ni jambo la kusubiri wakati “Mwalimu amekiandaa kikosi chake na kipo sawasawa kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Ruvu Shooting,  mchezaji mmojammoja yupo tayari kuona anapata pointi tatu mbele ya wapinzani wetu.

 

“Kikubwa tunawaomba mashabiki wajitokeze kwenye mchezo wetu ambao ni mgumu na wenye ushindani mkubwa,” alisema.

 

Naye Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire, amesema kuwa kitakachowaponza Yanga kwenye mchezo wao wa leo ni uwepo wa Kocha Charles Boniface Mkwasa kwenye benchi la timu yao ambaye anaijua vizuri Yanga.


 

“Yaani hao Yanga hata sijui wanaponea wapi? Kwa sababu ukiachilia mbali soka letu kubwa na la kutisha tunalocheza, tunaye kocha Mkwasa Master, ambaye yule ile Yanga yote ipo kwenye mkono mwake, anaijua vizuri sana, sasa najaribu tu kuwaza watatokaje.

 

REKODI INAYOSAKWA


 Unaambiwa kama Yanga wakiibuka na ushindi wowote leo, timu hiyo itakuwa inazidi kuweka rekodi za aina yake, ushindi kwa Yanga  utawafanya kuweka rekodi ya kucheza michezo 27 bila kupoteza.

 

 

Yanga kwa sasa imefikisha idadi ya michezo 26 mfululizo bila kupoteza kuanzia Machi 15, 2020, Yanga bado inaifukuzia rekodi ya Simba ambayo waliiweka ya kucheza mechi 33 bila kupoteza kutoka Aprili 10, 2017 hadi Mei 12, 2018.

3 COMMENTS:

  1. mechi ishauzwa hiyo

    ReplyDelete
  2. Ukiteleza Mnyama atachanja mbuga

    ReplyDelete
  3. Wabongo bwana nunueni na ninyi maana Yanga akishinda kanunua mechi ila Simba anashinda kihalali nunuen na ninyi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic