LICHA ya kubanwa mbavu nyumbani, lakini imekuwa faida kubwa kwa Simba na kusonga hatua ya kwanza ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.
Jana Desemba 5, Simba ikiwa Uwanja wa Mkapa jijini Dar, ilishindwa kufungana na Plateau United ukiwa ni mchezo wa marudiano wa michuano hiyo na kuifanya Simba kusonga hatua inayofuata kwa faida ya bao la ugenini.
Kusonga mbele kwa Simba, kumewaibua mashabiki wa timu hiyo wakiwaambia wapinzani wao, Yanga kwamba: “Si mliwaleta Plateau, mkawapokea vizuri pale uwanja wa ndege, sasa waleteni wengine, sisi tumesonga mbele.”
Katika mchezo wa kwanza uliochezwa wikiendi iliyopita nchini Nigeria, Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Clatous Chama ambapo bao hilo limekuwa na faida kubwa kwao baada ya jana kupata matokeo ya 0-0.
Kwenye mchezo wa jana,Simba inabidi wajilaumu wenyewe kwa kushindwa kupata mabao kwa kuwa walitengeneza kona 12 ambazo hazikuweza kuleta matunda.
Kiungo wa Simba, Luis Miquissone, alifanya jaribio moja kali ndani ya 18 dakika ya 74 likiwa ni jaribio la pili ambapo la kwanza lilipigwa na Hassan Dilunga dakika ya 60 liliokolewa na kipa wa Plateau United, Adam Abulari.
Mara ya mwisho Simba kufungwa nyumbani katika michuano ya CAF ilikuwa mwaka 2013 katika Ligi ya Mabingwa Afrika walipocheza dhidi ya Recreativo do Libolo ya Msumbiji, wakifungwa 1-0.
Jinsi Simba alivyobanwa mbavu?! Mbona unachekesha? Takwimu ulizoleta zinaonyesha Simba ndiyo walikuwa na mkono wa juu. Pili ushindi kwa Simba jana ilikuwa ni kuepuka kupoteza mchezo ambacho ndo walichofanya. Plateau walilazimika kushinda zaidi ya bao mmoja. Hivi hapa aliyebanwa mbavu ni nani? Kichwa cha habari kimekaa kushabiki zai
ReplyDeletedi kuliko hali halisi iliyotokea uwanjani.
Waandishi wetu bure kabisa, upendeleo hata kwenye jambo la wazi!!
DeleteSimba imebanwa mbavu wakati ndio waliotoboa raundi ya pili? Huu kama si ukanjanja wa aundishi wa habari kitu gani?
DeletePosession 55 kwa 45.Kona 12 kwa 0.
ReplyDeleteSijui aliyebanwa mbavu ni nani?
Waandishi wa Utopolo.
Hili ni jambo la aibu kwa tasnia ya uandishi wa habari. Hivi mwandishi anakosa hata uzalendo katika taarifa yake anayohabarisha umma dàh... Na mhariri wake kakaa kimyaaaa wala hakemei upotoshaji huo....😔🙄🤯
ReplyDeleteHuyu mwandishi hajielewi. Au ana mrengo ule wa wakarimu wageni. Awahi airport kusindikiza
ReplyDeleteIngekuwa kweli imebanwa Simba isingetoka kifuwa mbele NA kupata nafasi ya kukata mbuga
ReplyDelete