UONGOZI wa
klabu ya Yanga chini ya Mwenyekiti Dkt. Mshindo Msolla leo Desemba 7 umefanya uteuzi wa wanachama nane akiwemo Mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo, Imani Madega kuunda
Kamati ndogo ya mabadiliko ya Katiba Yanga.
Madega aliwahi kuiongoza Yanga kwa miaka mitatu katika nafasi ya Uenyekiti tangu mwaka 2007 hadi mwaka 2010.
Pia amewahi kuhudumu kwenye Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) akiwa mjumbe wa Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji.
Ikumbukwe kuwa Jumatano ya
Novemba 2, mwaka huu kampuni ya La Liga ilikabidhi rasmi rasimu ya mabadiliko
ya uendeshaji wa klabu hiyo ambayo inataka kubadili mfumo na kujiendesha
kisasa.
Wajumbe
wengine walioteuliwa kuunda kamati hiyo ni; Wakili Raymond Wawa (Mwenyekiti),
Wakili Sam Mapande, Wakila Audats Kahendagile, Wakili Mark Anthony, Mohammed
Msumi, Pastory Kiyombia na Debora Mkemwa.
Hao wamechunjwa pasipo shaka ni wananchi? Otherwise......,,,
ReplyDelete