January 15, 2021

 


NYOTA wa zamani wa kikosi cha Azam FC, Yahya Zaid aliyekuwa anakipiga nchini Misri amerejea kwa mkopo ndani ya maskani yake ya zamani.

Zayd alisepa ndani ya kikosi cha Azam FC baada ya kupata dili nchini Misri kwenye Klabu ya Ismaily msimu wa 2018 ambapo mabosi wake hao walimtoa kwa mkopo akakipige ndani ya Pharco.

Kutokana na ugumu wa namba ndani ya kikosi hicho ambacho alikuwa anacheza mzawa huyo wa Morogoro aliamua kuomba aondoke jambo lililomfanya afikirie kurejea Azam FC.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa wamekubaliana kumchukua mchezaji wao wa zamani kwa kuwa alikuwa ndani ya timu hiyo na anajua falsafa za Azam FC.

"Tumemalizana na Zayd kwa mkopo wa miezi sita na kwenye mkataba wake kuna kipengele cha kuweza kumchukua jumlajumla ikiwa kutakuwa na maelewano ya pande zote mbili.

"Kikubwa ni kuona kwamba kunakuwa na maelewano ya pande zote mbili ili tuweze kufikia makubaliano ya kubaki na mchezaji huyo ndani ya Azam FC," .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic