January 15, 2021

 


UONGOZI wa Simba umetambulisha utatu mpya ambao utapeperusha bendera ya Tanzania kimataifa katika Ligi ya Mabingwa Afrika. 

Imekuwa ikielezwa kuwa Klabu ya Simba inayonolewa na Kaimu Kocha, Seleman Matola ipo kwenye mpango wa kumsajili nyota wa Klabu ya FC Platinum, Perfect Chikwende.

Winga huyo amekuwa maarufu ghafla baada ya kuitungua Simba kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa hatua ya mtoano uliochezwa Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe. 

Nyota huyo amekuwa akitajwa kuibukia ndani ya Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina ambayo imemalizana na mshambuliaji Mpianza Monzinizi kutoka FC Lupopo na kipa Mathias Kingonya.

Usajili wa kipa huyo unatajwa kuweza kumuondoa kipa mmoja ambaye ni David Kissu pamoja na mshambuliaji mmoja ambaye ni Richard Djod.

Ikiwa Chikwende atamalizana na Simba ataungana na kiungo mshambuliaji Luis Miquissone na mshikaji wake Clatous Chama ambao wamekuwa wakifanya vizuri ndani ya Simba.

Kupitia Ukurasa wa Instagram wa Haji Manara, ameandika kuwa Chama +Chikwende + Miquissone =CCM



9 COMMENTS:

  1. Karibu Sana Chikwende ufurahie maisha ya soka ndani ya club kubwa na yenye malengo makubwa zaidi

    ReplyDelete
  2. Yeah true nature bab,waache waandamane kwa kuchukua kombe la mapinduzi sisi tutaandama kwa kuchukua ubingwa wa ligi kuu na kuingia robo fainali klabu bingwa Afrika hiyo ndo saizi yetu bro

    ReplyDelete
  3. Vipi Lwanga maana badala ya kukimbia ananyata ,Lile meo,mapinduzi imekuuma Sana ,subiri vifaa viwili ndo mtalia

    ReplyDelete
  4. Unaonekana una hasira Kila ukifikiria kombe lenyewe mlilochukua unazidi kukereka na hivyo vifaa viwili sijui mpaka Sasa ushachangia shilingi ngapi ya kuvipata

    ReplyDelete
  5. Hivyo vifaa viwili isije ikawa Sarpong na Yipke waliochangamka

    ReplyDelete
  6. Je wale Wahindi/Wabrazili eti mbona huwataji?

    ReplyDelete
  7. Ndugu zake CEO wenu nasikia wajomba zake

    ReplyDelete
  8. Hivi eti Barbara alitaka kubakwa msikitini?! Wapi hapo alipokuwa anaswali pekee?

    ReplyDelete
  9. Chikwende hawezi kucheza caf league
    Ma huyu anayechomeka suala la ceo kubakwa linauhusiano gani na topic husika au ndio mbakaji mwenyewe?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic