Mbeya City imekamilisha usajili wa wachezaji watano huku Barthez aliyehudumu kwa vipindi tofauti kwenye vikosi vya klabu za Simba na Yanga akiwa amesaini kandarasi ya miaka miwili.
Msimu uliopita Barthez alihudumu katika kikosi cha klabu ya Ndanda kabla timu hiyo haijafikia uamuzi wa kuachana naye mwishoni mwa msimu.
Akizungumzia usajili wake, Barthez amesema: “Nashukuru kujiunga na klabu hii, najua kuna wajibu mkubwa mbele yangu wa kushirikiana na wachezaji wenzangu ili kuinusuru timu kutoka katika hatari ya kushuka daraja, naamini bado tuna michezo mingi na tunaweza kufanya vizuri kwenye michezo ya mzunguko wa pili,”
Kwenye Ligi Mbeya City inakamatia nafasi ya 17 katika msimamo ikiwa imejikusanyia pointi 14 tu katika michezo 18 waliyocheza mpaka sasa.
0 COMMENTS:
Post a Comment