January 16, 2021


 KIKOSI cha Azam FC kimefunga usajili wa dirisha dogo kwa kuinyaka saini ya kiungo mshambuliaji, Yahya Zayd, kwa mkopo wa miezi sita akitokea Pharco ya Misri.


Zayd ni mmoja wa wachezaji waliokulia kwenye kituo cha Azam Academy kabla ya kumpandisha timu kubwa ya Azam FC na aliuzwa katika Klabu ya Ismaily ya Misri 2018.

Kiungo huyo mshambuliaji anfunga usajili wa dirisha dogo akiungana na mshambuliaji Mpiana Monzinzi (Congo DR) na kipa Mathias Kigonya (Uganda).

Azam imeachana na kiungo mshambuliaji Richard Djod mzee wa udambwiudambwi ambaye ameachwa ili kupisha nafasi ya kipa Kigonya.

Awali ilikuwa inaelezwa kuwa kipa namba moja David Kissu angetolewa kwa mkopo ila mambo yamekuwa tofauti baada ya Kocha Mkuu, George Lwandamina kuamua abaki ndani ya timu hiyo.

Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria amesema kuwa malengo ya Azam FC ni kufanya vizuri ndani ya Ligi Kuu Bara pamoja na mashindano mengine.

3 COMMENTS:

  1. Kikubwa Dana Azamu mnatunyima raha sisi mashabiki.tunaomba mtwae ubingwà ndo raha yetu sisi

    ReplyDelete
  2. Pia maoni yangu naomba mtue ubingwa was vodacom premier league au shirikisho ili kurejea ushindani wa kimataifa ndo furaha yetu sisi maana sasa ivi mnatunyima raga kwakuwa hamtwai ubingwa

    ReplyDelete
  3. Hawana jipya hao azam badala ya kusajli wanatania

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic