January 17, 2021

 KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison amesema kuwa miongoni mwa vitu ambavyo anavikumbuka ndani ya Simba ni pamoja siku yake ya utambulisho iliyofanyika siku ya Simba day.

Nyota huyo aliibuka ndani ya Simba akitokea Klabu  ya Yanga ambapo dili lake limekuwa na utata hasa suala lake la mkataba.

Mabosi wake wa zamani Yanga wanadai kwamba mchezaji huyo ni mali yao kwa kuwa alisaini dili la miaka miwili huku yeye akiweka wazi kwamba alisaini dili la miezi sita. 

Sakata lake lilitinga Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) ambapo lilisikilizwa kwa muda wa siku tatu kisha ikaamuliwa kwamba mchezaji huyo ni huru kwa kuwa kulikuwa na makosa ya kimkataba ikiwa ni pamoja na suala la saini na mhuri.

Morrison amesema:"Ninaikumbuka siku ile ya utambulisho kwa mashabiki, Uwanja wa Mkapa, namna ambavyo walinipokea na kunishangilia ilikuwa furaha kwangu na ipo kwenye kumbukumbu zangu, " .

Kwa sasa ndani ya Simba amekuwa hana nafasi kikosi cha kwanza huku ikielezwa kuwa ana matatizo ya afya jambo ambalo linamuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu.

3 COMMENTS:

  1. Tunakuombea upone na irejee hali yako iwe kama ulivo kuwa kabla kuumwa na uichezee Simba kwa furaha na mafanikio makubwa uyasahau machunngu yako yote

    ReplyDelete
  2. Inawezekana Yanga wamefanya mambo yao? Maana walisema Morrison hatacheza mpira huko Simba, na sasa tunasikia anaumwa ngiri.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic