KOCHA Msaidizi wa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania,Taifa Stars, Seleman Matola amesema kuwa ni jambo la msingi kwa Watanzania kuendelea kuipa sapoti timu ya Taifa ili wachezaji waweze kufanya vizuri.
Kwa sasa kikosi cha Stars kipo nchini Cameroon kwa ajili ya kushiriki michuano ya CHAN 2021 ambayo inashikirisha wachezaji wa ndani.
Taifa Stars maandalizi yao yanafanyika kwenye Uwanja wa Centenary, Limbe nchini Cameroon kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya Chan ambapo wataanza kutupa kete ya kwanza Januari 12 dhidi ya Zambia.
Matola ataungana na kikosi leo pamoja na beki kiraka Erasto Nyoni ambaye alikuwa na matatizo ya kifamilia.
Akizungumza na Saleh Jembe, Matola amesema:"Jambo la msingi ni kwa Watanzania kuipa sapoti timu ya Taifa ya Tanzania, imani yetu kubwa ni kwamba tutafikia malengo kwa kuwa kila kitu kinawezekana," .
January 12 itakuwa mwaka kesho au mana sielewi elewi hapo!
ReplyDeleteHahaha msamehe bure kachapia huyo
ReplyDeleteSasa Matola anaondoka halafu timu ya simba itasimamiwa na nan.
ReplyDeleteSasa Matola anaondoka timu ya simba itasimamiwa na nan.
ReplyDelete