January 30, 2021


 UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa zawadi atakazopata bingwa wa michuano ya Simba Super Cup iliyoanza Januari 27, 2021 ni fedha taslimu shilingi milioni 15, kikombe na medali.

 Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wamepanga kutoa zawadi hiyo pamoja na kutoa burudani kwa mashabiki ambao watajitokeza kutazama mashindano hayo ambayo ni mara ya kwanza kufanyika ndani ya ardhi ya Bongo.


Katika mashindano hayo ni timu tatu ambazo zinashiriki ikiwa ni Simba wenyewe ambao ni wenyeji, Al Hilal ya Sudan na TP Mazembe ya Congo.


Simba ilianza mchezo wa ufunguzi Januari 27 na ilishinda mabao 4-1 dhidi ya Al Hilal na mchezo wa pili ulikuwa ni jana, Januari 29 ambapo Al Hilal ilishinda mabao 2-1 dhidi ya TP Mazembe.


Kilele ni kesho Januari 31 ambapo Simba itacheza na TP Mazembe na mshindi atapatikana kesho, Uwanja wa Mkapa.


Manara amesema baada ya mchezo wa mwisho kutakuwa na tafrija (after party) ambayo itafanyika ‘Kidimbwi Beach’ jijini Dar es Salaam.


Na siku hiyo kutakuwa msanii wa Bongo Fleva Zuchu ambaye katika mchezo wa mwisho wa michuano hiyo utakaopigwa Jumapili, Januari 31, 2021 kati ya Simba vs TP Mazembe atatoa burudani.

 

Manara amesema:-"Tumejipanga na tunawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kushangilia na kuona burudani, pia atakuwepo Zuchu ambaye yeye mwenyewe amesema kuwa mchezaji anayemkubali ni Aishi Manula ila siyo kumzimia maana nyinyi hamuishiwi maneno.


"Ila hata kama akimzimia hakuna tatizo Manula anajulikana na ni miongoni mwa watu ambao huwa wanaandamwa wakifanya makosa licha ya kwamba ni kijana mtaratibu," .

2 COMMENTS:

  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  2. Very good and all the best to my club.
    SIMBA NGUVU MOJA.
    🦁💪🏾1️⃣🇮🇩⚽🔥

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic