BAADA ya kufungiwa miaka mitatu kujihusisha na shughuli za mpira wa miguu ndani na nje ya nchi na Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa hajaridhishwa na hukumu hiyo hivyo atawakilisha rufaa yake.
Kamati hiyo ilimpa adhabu hiyo Bumbuli baada ya kushindwa kulipa kiasi cha Sh. 5,000,000 kama ilivyoainishwa kwenye hukumu yao iliyotolewa tarehe 28 Septemba 2020, baada ya kiongozi huyo kukutwa na hatia.
Taarifa ya kamati hiyo ya maadili iliyotolewa, 27 Januari 2021, imeeleza kuwa adhabu ya kumfungia kiongozi huyo kwa kipindi cha miaka mitatu imetolewa chini ya cha 73(8)(a) cha mwongozo wa maadili ya TFF, toleo la 2013.
Akizungumza baada ya adhabu hiyo Bumbuli amesema kuwa hukumu hiyo imeshatoka na wameipokea ila kwa upande wake bado hakuridhika na maamuzi hayo na atakata rufaa.
“Nyundo imeshuka na tumeshaipokea na tutaijadili na uongozi wa Yanga tujue tunafanyaje, na kiufupi hatukuridhika na hukumu ilivyotoka kama ilivyokuwa ya awali na tutakata rufaa ambayo tutaiwasilisha hii leo,” amesema Bumbuli.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa amesikitishwa na hukumu ya kufungiwa kwa Bumbuli kwa kuwa alikuwa anapenda kuendelea kufanya kazi na ofisa huyo kwenye sekta ya mpira hivyo anamuombea aweze kurejea kazini.
Wazee wa yanga wamesema wataandama hadi TFF kupinga haya maamuzi. Nahisi watafanya hivyo na ndumba zao kiunoni ili kurahisisha kupata maamuzi chanya kwao.
ReplyDeleteHAPO DAWA NI KULIPA FAINI TU NA SIO MAANDAMANO, AMELETA DHARAU UNSFIKIRI WAKINA KIDAU WATAMSAMEHE? LAZIMA APIGWE NA NYUNDO YA UTOSI TU. NGOJA TUONE
ReplyDelete