January 30, 2021


 FISTON Abdulazack, mshambuliaji mpya ndani ya kikosi cha Yanga amesema kuwa sababu kubwa ya kusaini mkataba ndani ya timu hiyo ni ukubwa wa timu hiyo.

Nyota huyo ambaye ni raia wa Burundi jana Januari 29 alitua Bomgo kumalizana na mabosi wake hao na amesaini dili la miezi sita. 

Yeye ni mshambuliaji anaungana na kiungo mshambuliaji, Said Ntibanzokiza ambaye tayari ameshaanza kutumika ndani ya kikosi hicho akiwa amecheza mechi mbili za Ligi Kuu Bara. 

Fiston amesema:"Nimesaini Yanga kwa kuwa ni timu kubwa na inajulikana nje na ndani ya nchi hivyo nami nimekuja pia kuungana na timu hii.

"Najua wengi wanapenda kuona nitafanya nini wasiwe na mashaka nitafanya vizuri na kila kitu kitakuwa sawa, ".

Yanga ipo nafasi ya kwanza chini ya Kocha Mkuu,  Cedric Kaze ina pointi 44 baada ya kucheza mechi 18 ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21.

8 COMMENTS:

  1. Daima mbele nyuma mwiko...

    ReplyDelete
  2. Your most well come to join with other stars

    ReplyDelete
  3. Wayanga wenzangu tukumbuke amesain miezi sita huyo yasije yakawa ya morison

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mbona Morison alikuwa na mkataba wa pili wa miaka 2. Ni uhuni tu umetumika... subiri utaamini ninachosema

      Delete
  4. Simba ni wahuni tu walifanya kuharibu mambo ila laana ya hili jambo itawangukia tu

    ReplyDelete
  5. Utopolo mmesajili wachezaji 10 wa kigeni bado mnamtaka Morisson!!
    Utopolo sheria hamfuati mkipigwa nyundo mnabaki kulalama.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic