MSHAMBULIAJI hatari wa kikosi cha klabu ya Azam, Prince Dube amefungukia usajili wa beki mpya wa Simba raia wa Zimbabwe, Peter Muduhwa kwa kusema ni mchezaji mzuri na anaamini kwa kiwango chake Simba hawatajutia kumsajili.
Muduhwa amekamilisha
usajili wa kujiunga na Simba akitokea kikosi cha Highlanders FC ya Zimbabwe
ambapo amewahi kucheza na Prince Dube.
Muduhwa alikuwa sehemu ya
kikosi cha Zimbabwe kilichokuwa kikishiriki michuano ya kombe la mataifa ya
Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN).
Muduhwa amekuwa mchezaji wa
tano kusajiliwa na Simba katika kipindi cha dirisha dogo baada ya Taddeo
Lwanga, Doxa Gikanji, Tatenda Chikwende na Junior Lukosa ambapo timu hiyo
inaonekana kujiimarisha kwa ajili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kombe
la Ligi Kuu Bara.
Akimzungumzia beki huyo
Dube alisema: “Kwangu ni jambo la furaha kuona ndugu yangu mwingine akija
Tanzania, nampongeza kaka yangu Muduhwa kwa kukamilisha usajili wake Simba.
“Ni mchezaji mpambanaji na
wa kiwango cha juu, naamini atakuwa msaada mkubwa kwao na namtakia kila la
kheri kwenye majukumu yake mapya,”
Sawa, ngoja tumuone
ReplyDeleteNaomba kueleweshwa Simba imesajili wachezaji wakigeni zaidi ya kumi kinyume na kanuni za tff he hawawachezaji watacheza ligikuu?
ReplyDeleteUwe unafatilia michezo wachezaji kumi ni wa ligi hao wengine wanatumika kwenye michuano ya klabu bingwa.
DeleteHalafu waulize utopolo kwanini wamesajili wachezaji kumi halafu Morison wa kumi na moja wanadai wao
Kunazidi kunoga Simba. La Africa mfike mbali na ubingwa wa nyumbani ubaki hapohapo mukamilishe misimu mine na tuzidi kuendelea nalo Mpaka wasalimu amri
ReplyDeleteKunazidi kunoga Simba. La Africa mfike mbali na ubingwa wa nyumbani ubaki hapohapo mukamilishe misimu mine na tuzidi kuendelea nalo Mpaka wasalimu amri
ReplyDeleteSwafi
ReplyDelete