KOCHA Mkuu wa
Yanga, Cedric Kaze ameonyesha hataki mchezo ndani ya kikosi hicho kufuatia
kuwataka nyota wote wa kikosi hicho akiwemo kiungo mshambuliaji, Saido
Ntibazonkiza kuhakikisha wanaulinda uzito waliokuwa nao katika kipindi hiki na
iwapo mchezaji yeyote kati yao ataongezeka uzito atapigwa faini.
Wachezaji wa Yanga wamepewa mapumziko hadi Jumatatu tarehe 25 ndipo kikosi kitarejea kambini kwa ajili ya maandalizi ya ligi inayotarajia kurudi tena mwezi Februari.
Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinasema kuwa, benchi la ufundi la timu hiyo limewapima uzito nyota wote kabla ya kwenda katika mapumziko mafupi na kuagiza kuwa iwapo mchezaji yeyote atarudi na uzito tofauti na ule alioondoka nao basi atapigwa faini kutokana na kutozingatia program aliyopewa na kocha.
“Kocha amezungumza na wachezaji na amewataka kuhakikisha kila mmoja anakuwa makini kwa kuzingatia uzito wake, kwa kuhakikisha hawali vitu vyenye sukari nyingi pamoja na vyenye protini nyingi ili kuhakikisha wanakuwa katika uzito ule anaoutaka kocha.
“Awali wachezaji hao walipimwa wakati wanakwenda katika michuano ya kombe la Mapinduzi kujua uzito wa kila mmoja pia wamepimwa wakati wanakwenda kwenye mapumziko, na kila mmoja ameondoka akiwa anajua ana uzito wa kiasi gani hivyo ikitokea mmoja wapo ameongezeka zaidi ya hapo basi atapewa adhabu kwa kuwa tayari wameshapewa tahadhari na nini cha kufanya," katika kipindi hiki kwa kutojiachia kila mmoja anatakiwa azingatie kiwango chake.”
0 COMMENTS:
Post a Comment