UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa bado una matumaini na kipa wao namba moja David Kissu licha ya kupitia kipindi kigumu ndani ya timu hiyo kwa sasa.
Awali ilikuwa inaelezwa kuwa Kissu angesepa ndani ya kikosi hicho kwa mkopo huku timu ambayo ilikuwa inapewa nafasi ya kumchukua ni Biashara United.
Azam walikuwa wanahusishwa kusepa na kipa wa Biashara United ambaye yupo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ambayo kesho itamenyana na Zambia kwenye mashindano ya Chan, Cameroon.
Hivyo kama dili la kumvuta Mgore lingekamilika huenda Kissu angeibukia Biashara United kupiga kazi na Francis Baraza.
Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit aliweka wazi kuwa timu hiyo haina mpango na Mgore zaidi ya kuwa ni tetesi tu.
Kuhusu ishu ya Kissu, Thabit amesema:"Kawaida kwa makipa kufungwa haina maana kwamba ukiwa unafungwa wewe sio bora hapana kila kitu ni suala la muda.
"Uwezo wake ni mkubwa kwani huwezi kusahau kwamba kuna wakati aliweza kufanya vizuri mfululizo na kuifanya timu kuwa nafasi ya kwanza.
"Anayopitia kwa sasa ni sehemu ya kazi imani yetu atakuwa bora na hakuna mpango wa kumuondoa kikosini," .
Juzi ikiwa visiwani Zanzibar, Azam FC ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya KMMK ikiwa ipo kwenye maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho.
Kwenye mashindani ya Kombe la Mapinduzi, Kissu alikuwa jukwaani akiwashuhudia Benedick Haule na Wilbol Maseke wakiwa langoni.
0 COMMENTS:
Post a Comment