KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars ,Etienne Ndayiragije amesema kuwa maandalizi ya kikosi hicho nchini Cameroon yapo sawa na wana amini wataanza vizuri kesho.
Stars ikiwa imeweka kambi nchini Cameroon kwa ajili ya mashindano ya Chan ambayo ni maalumu kwa ajili ya wachezaji wa ndani kesho kitaanza kazi yake dhidi ya Zambia.
Mazoezi ya Stars yanafanyika Uwanja wa Centenary,Limbe nchini Cameroon ikiwa ni maalumu kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya CHAN.
Tayari kiraka Erasto Nyoni ambaye hakuwa na kikosi awali kutokana na matatizo ya kifamilia ameshatia timu Cameroon jana pamoja na kocha msaidizi, Seleman Matola alikuwa na timu ya Simba kwenye Kombe la Mapinduzi ambapo huko alishika nafasi ya pili baada ya ubingwa kuwa mali ya Yanga.
Ndayiragije amesema:"Ilikuwa kazi kubwa kwenye mchezo wetu wa kirafiki dhidi ya DR Congo ila kwa sasa makosa yetu tumeyafanyia kazi.
"Tunaamini kwamba haitakuwa rahisi lazima tupambane, nimewaambia vijana kwamba kazi yetu ni moja kusaka ushindi ndani ya uwanja," .
Mchezo huo utachezwa saa 1:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Kila lakheri Taifa Stars,
ReplyDelete