January 24, 2021

 

FISTON Abdoul Razak nyota mpya wa Klabu ya Yanga amesema kuwa Yanga hawatakuwa na haki ya kumzuia kuondoka ikiwa atafanya vizuri ndani ya kikosi hicho baada ya kusaini dili la miezi sita.

Nyota huyo raia wa Burundi amesaini dili la miezi sita katika usajili wa dirisha dogo uliofungwa Januari 15,2021 kwa ajili ya kuongeza nguvu ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze.

Anaungana na nyota mwingine, Saido Ntibanzokiza ambaye naye pia ni raia wa Burundi ambaye huyu anatajwa kusaini dili la miaka miwili.

Habari zinaeleza kuwa Fiston ambaye ni mshambuliaji mwenye uwezo wa kucheza pia nafasi ya winga anasubiri dili lake jingine litiki nchini Kuwait.

"Miezi sita kwangu ni sawa itanipa fursa ya mimi kuondoka bila kuzuiwa pale ambapo nitahitaji hivyo nina amini nikifanya vizuri itakuwa njia kwangu ya kuondoka.

"Ila kwa namna ambavyo nimeiona Yanga nina amini nitaongeza mkataba mwingine wa kusalia ndani ya kikosi hicho," amesema.

Yanga ambao ni mabingwa wa Kombe la Mapinduzi kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara wapo nafasi ya kwanza na pointi zao ni 44.

22 COMMENTS:

  1. Mkwara huo, maana anajua yaliyompata maskini Morisson. Kijana wa watu katengenezewa mkataba feki na kurogwa juu. Watu wana rogo mbaya jamani.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hangaikeni na zigo lenu la miba mmebaki kumwaga povu tu ooh kapigwa misumari sijui Yanga roho mbaya si mtafute nyundo muichomoe!!

      Delete
    2. Nyie so ndo mlikuwa mnajisifia kuea mmemroga Leo hii baada ya kusikia yupo fiti mnaanza kuweweseka eti hangaikeni na zigo lenu subiri jmatno ukimuona anavyoupanda Mpira kijuso kitakuwa kidogo Kama pilitoni

      Delete
    3. kuupanda mpira ndio Kombe la club bingwa africa ebu tueleze wewe team nyau mweusi

      Delete
  2. Yanga ijiweke tayari kwani akitokea mwenye kiwango, mambo yatakuwa kama yale ya Morison na kusingizia kuwa kapewa mkataba wa miaka miwili hamtoweza kujiripiti tena na wenye hela ya hakika ndio itakuwa mali yao

    ReplyDelete
  3. Inaonekana jamaa mzuri "uleeee",mmeanza kuchungulia bravo scouting Team ya Yanga inatisha ,mikia mnamtolea udenda .Nimegundua ndiyo maana kuna Cr7 na Messi.Kumbe unaweza kununua mitumba Baro moja ukaambulia nguo kumi nzuri zilizobaki ukaambulia lonya,Lakini anayenunua mpya anaona habahatishi. Kwahiyo hapo nauliza kwanini Fiston anafuatwa Sana mbona lonya zilizo letwa pande nyingi hasa pale jirani hamtupi upadate?.Vipi Lwanga amepewa muda gani wa kuwa fiti?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kweli scouting si ndo Mana mkaleta Yipke mkaleta Sarpong,mkaleta wanariadha na saivi mnaongoza ligi kwa tofauti ya point kumi,mmeingia hatua ya makundi klabu bingwa Afrika,mmechukua kombe la mapinduzi kweli scouting yenu noma

      Delete
    2. Aliyekwambia anamtaka huyo Sarpong aliyechangamka Nani,nyie endeleeni kujifariji tu na Ayo magarasa yenu alafu baadae muwasingizie TFF ni Simba wakati round ya Kwanza asilimia 65 mmebebwa

      Delete
    3. Huyo si ndo anang'ang'ania Simba ipo round ya pili,Yani timu imeingia hatua ya makundi baada ya kuvuka round ya pili alafu mtu anakwambia Simba ipo round ya pili Sasa huyo si mwehu

      Delete
  4. Hawajui uto huyu tangu lini wakaachia mchezaji

    ReplyDelete
  5. Inaonekana huyo keshaekewa uwanjani mkwanja mzito na si mtu wa kuchezewa ovyo ovyo.

    ReplyDelete
  6. Mimi nazidi kuwasaidia Simba imeingia last 16 siyo robo finali angalia hata namba,huu mfumo wa makundi uliyopo hauna miaka hata minane toka uanze Kama sikosei ,mlianza round ya awali huo ndiyo ukweli mkawatoa Platnum round ya kwanza .Kwangu tukana usitukane ukweli ndiyo huo .Pili Sarpong na Mugalu yupi meo na Kama mnawachezaji siyo Vimeo kwanini mnasajili ?eti Corona wale Wahindi watatu wapo wapi au yule ajuza wa Kisudan ?

    ReplyDelete
  7. Mpo round ya pili ambayo kwa mfumo wa sass ni group stage,mkipita hapo ni last eight(8) au quarter final group stage vilevile ya Timu nne kila kundi ,halafu mbili zitapita kila kundi yaani Timu ya kwanza na ya pili kila kundi A na B Hiyo ni last 4 (nusu fainali)hii uchezwa knockout home and away mshindi wa kwanza group A anacheza na wa pili group B na mshindi wa pili group A anacheza na mshindi wa kwanza gruop B then washindi (last two wanacheza fainali huelewi kampe Haji akusaidie maana kawakamata akili akisema yeye hope utaamini

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tofautisha makundi na mzunguko, kama hujui lugha piga kimyaa, vyura kwaO majini, nchi kavu sio kwenu

      Delete
  8. Wewe chizi Kila siku unaambiwa Simba imevuka round ya pili imeingia group stage imeshavuka round ya pili walicheza na Platinum Kama bichwa lako maji halielewi halafu kuhusu Mugalu na Sarpong Yani kweli ndo nazidi kuamini we chizi Mugalu anafunga karibu Kila mechi anayopewa nafasi uje kumfananisha na Sarpong kweli we ndimu maji

    ReplyDelete
  9. Eti quarter final ya group stage,kwenye quarter final Kuna group stage Tena ndo Mana tunasema Aya Mambo mtu alikuwa mlevi wa gongo alafu baadae kaacha anaona starehe ni Mpira ana uvamia tu kupitia mitandao ya kijamii,YouTube akuna chochote anachokijua

    ReplyDelete
  10. Kijana Kama una akili ya kutoelewa rudi Shule Elimu haina mwisho ingia African club champions league history utakuta Wikipedia Soma bt huko ni Kingereza toa akili ya kushikiwa na utake usitake mpo last 16 Kama wewe siyo mwendawazimu uliwahi kuona quarter final ya Timu 16 nakusaidia hili ubongo wako ukue mlvyowatoa Platnum imeenda upande wa Confederation ,zipo Timu 16+16=32 huko ndiyo second round huku club Bingwa mnacheza preliminary na First round mnakwenda group stage usiwe na bichwa gumu kuelewa Kama nyumbu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tulia uelimishwe mbwiga wewe, Simba kwa Sasa ipO hatua ya makundi 16 bora wakifuzu wanaingia 8 bora yaani robo fainali na wakishinda wanaenda 4 bora yaani nusu fainali, wakishinda wanacheza fainali, wakishinda wanakuwa mabingwa, watasubiri kushiriki mashindano ya klabu bingwa ya Dunia

      Delete
  11. Nimekosea Timu mbili za makundi Yale manne ya kwanza na ya pili jumla nane zitacheza mtoano (manake robo fainali)zibaki nne(nusu fainali )kumbuka mlivyotolewa na Mazembe mwaka juzi hakuna makundi Tena Lkn naendelea kusisitiza hampo robo fainali mpo round ya pili inayoendeshwa kimakundi

    ReplyDelete
  12. mbululaz ziko nyingi mno huku ndio maana mnazimiwa net

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic