January 24, 2021


 MWINYI Zahera aliyekuwa kocha ndani ya Klabu ya Yanga kabla ya kuchimbishwa msimu wa 2019/20 amesema kuwa Simba hawana mkwanja wa kumchukua Florent Ibenge awe mbeba mikoba ya Sven Vandenbroeck.


Imekuwa ikielezwa kuwa Ibenge amepewa dili na mabosi wa Simba akitokea Klabu ya AS Vita ya Congo pia anafundisha timu ya Taifa ya Congo.

Ibenge amesema kuwa kweli aliwahi kuzungumza na Simba kuhusu kuhitaji huduma yake ila mazungumzo yao hayakufika sehemu nzuri.

Zahera ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi ndani ya Klabu ya Gwambina FC amesema haitakuwa rahisi kwa Ibenge kuibuka ndani ya Simba.

"Simba hawana pesa ya kumchukua Kocha Florent Ibenge kuwa kocha wao mkuu,wanaosema hivyo waongo.

"Ibenge ni kocha mzuri ila hawezi kuja kwa Simba, najua hawana hela ya kumchukua kocha huyo kwa sasa," .

19 COMMENTS:

  1. PUMBAVU ZAKO ZAHERA MACHO KAMA MIKUNDU YA KUKU

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndugu tumia lugha ya staha kufikisha ujumbe wako na utaeleweka vizuri tu kutukana kunaonesha wewe ni mtu aina gani kiasi kwamba sisi wachangiaji wengine tunachora picha akilini mwetu kuwa huenda umekosa malezi bora ya wazazi wako

      Delete
    2. Simba watachukua bora zaidi kuliko Ibenge.zahera mtu wa kuropokwa mambo asiyoyajua kama mitandao mingi ya habari za michezo hapa bongo.

      Delete
  2. Zahera naye kenge tuu. Kwani yeye ni msemaji wa ibenge au ni mke wa ibenge hadi aseme vile? Tunajua yeye ndio anamshawishi bwana wake asije simba kwa sababu ya vinasaba vyake na utopolo fc. Lama gwambina wanaweza kumlipa simba itashindwa kumlipa huyo basha wake?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sasa huyo Kenge kaja kwenu Mipaka fc,tukana tena!

      Delete
  3. Zahera anaikodolea macho nafasi ya kocha mkuu Simba lakini hawezi kuipata

    ReplyDelete
  4. Mimi najua ninyi watani wetu Simba,nilishawaeleza hamtaki msikie mtu yeyote anasema kinyume Cha mawazo yenu akisema tu tofauti kifuatacho ni matusi Tena mazito inasikitisha hata mwenye blog Ana publisize ,wakati nyingine Ana zi hariri ,nilicomment stage ya Simba the so called group nikasema second round kilichotokea matusi.Unajiuliza kwanini mtu ukihisi kakosea au kaenda kinyume nawe utukane?.

    ReplyDelete
  5. Wanazo pesa za kumchukuwa Ibenge na kesho utasema kuwa Simba hawana pesa za kukuchukuwa wewe. Ulimi jumba ya porojo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nadhani umepata jibu sasa. Simba wanatafuta hela na kwa sasa wamepata hela zaidi ya Billion moja kwa kuingia group stage.

      Delete
  6. Simba walishindwa kumbakiza Okwi, kutokana na dau lake, wataweza kumleta Coach wa viwango kama sio kudanganyana?
    Tatizo washabiki wamezoea kudanganyana ndio maana wanaambia kila kitu kinawezekana Ili wafurahi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tatizo sio dau, dau alilotaja Okwi lilikuwa linalingana na kiwango chake? Dau likilotumika kuwabakisha akina Miquisone na Chama ni maradufu ya alilohitaji Okwi. Lakini viongozi walikataa kwa Okwi na wamekubali kwa hawa wengine kwa sababu viwango vinashawishi.

      Delete
    2. Na ndiyo maana hata Yanga walikataa kutoa milioni zisizozidi 100 kwa Dante na Yondani ila wakakubali kutoa mil 180 kwa Mwamnyeto kwa sababu waliamini katika kiwango cha Mwamnyeto sio wale wawili

      Delete
  7. Kunatofauti ya kusema na kutendea, coach mzuri wa viwango anagharama zake, it's not simple like most of funs thinking...
    Endeleni kuishi kwa matumaini...

    ReplyDelete
  8. Mashabiki wa nyauuuu povu la kutosha,,,mnaambiwa ukweli hamuwezi,,,matusi yakutosha,,,mchukueni bac tuone

    ReplyDelete
  9. Simba kweli haina pesa pesa ni za No naona povu linawatoka paka fc.

    ReplyDelete
  10. Kulinganisha na YANGA au? Ma-star wa Simba wanalipwa kiasi gani? Kocha mpya kwa kuwaza kwako kaacha Al Merreikh kuja Simba kutalii au? Utopolo jiongeze katika kufikiri.

    ReplyDelete
  11. HAYAAAA SASA MWINYI ZAHERA NDIYE MKURUGENZI WA UFUNDIIIII

    ReplyDelete
  12. Mashabiki wa simba wana gubu hatare

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic