KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema kuwa anawatambua vema wachezaji wake wa timu hiyo hivyo hana mashaka katika mechi zake zijazo za Ligi Kuu Bara, Kombe la Shirikisho pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika.
Tayari Gomes raia wa Ufaransa ameanza kazi ndani ya Simba na kesho, Januari 27 anatarajiwa kuwa na mchezo wake wa kwanza ndani ya Bongo kwenye mashindano ya Simba Supe Cup.
Amerithi mikoba ya raia wa Ubelgiji, Sven Vandenbroeck ambaye alibwaga manyanga Januari 7 na kwa sasa yupo zake ndani ya Klabu ya FAR Rabat ya Morocco.
Januari 27 Simba itamenyana na Klabu ya Al Hilal ya Sudan ambayo inatarajiwa kutia timu leo kwenye ardhi ya Bongo.
Pia kipo kikosi cha TP Mazembe ambapo anakipiga pia Mtanzania, Thomas Ulimwengu kinatarajiwa kuwasili kesho kwenye ardhi ya Bongo kushiriki Simba Super Cup.
Gomes amesema:"Ninatambua kwamba kuna kazi kubwa ya kufanya ila hilo halinipi mashaka kwa sababu ninawatambua vema wachezaji wa timu hii na namna ambavyo wanacheza nina amini tutakwenda nao sawa.
"Ninapenda kuona kwamba timu inakuwa na umiliki wa mpira mkubwa hilo ni sehemu ya ushindi kwetu na namna wachezaji ambavyo wanapokea ninaona kwamba wanaelewa." .
Tunategemea mazuri kwako
ReplyDelete