KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Etienne Ndayiragije amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho, Januari 27 dhidi ya Guinea.
Stars ipo kundi D ambapo imecheza mechi mbili nchini Cameroon kwa ajili ya kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya Chan ambayo inawashirikisha wachezaji wa ndani.
Ina pointi tatu kibindoni na imepoteza pointi tatu baada ya kupoteza mchezo wake wa kwanza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Zambia, Uwanja wa Limbe.
Ikiwa itashinda kesho kwa ushindi wa namna yoyote itakuwa imekata tiketi ya kutinga robo fainali ya mashindano hayo yenye hadhi kubwa barani Afrika.
Itamkosa jumla beki mkongwe Erasto Nyoni ambaye amerejea Dar kutokana na kuwa majeruhi huku nyota John Bocco na Ibrahim Ame wakiendelea kuwa chini ya uangalizi.
"Tunajua kwamba mchezo utakuwa na ushindani mkubwa ila tunahitaji ushindi ili kusonga mbele. mashabiki watuombee ili tuweze kufanya kweli na kuweza kusonga mbele." .
Ushindi wa boa 1-0 dhidi ya Namibia unaifanya Stars iongeze nguvu ya kujiamini na nyota Farid Mussa ambaye alifunga bao hilo ana tuzo mkononi ya mchezaji bora kwenye mchezo huo.
Mchezo wa kesho itakuwa Uwanja wa Reunification uliopo kwenye mji wa Douala.
0 COMMENTS:
Post a Comment