January 26, 2021

 


LICHA ya kufutwa kazi ndani Chelsea, Frank Lampard ambaye alikuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo amesema kuwa ilikuwa ni heshima kwake kuwa Kocha ndani ya timu hiyo hivyo anashukuru kwa yote.

Lampard alifutwa kazi, Januari 25 na taarifa rasmi ilieleza kuwa ulikuwa ni uamuzi mgumu ambao mmiliki na Bodi ya Chelsea haikutaka kuufanya kwa kuwa matokeo hayakuwa bora hivi karibuni.

Alitangazwa kuwa kocha ndani ya timu hiyo Julai 4 na amekiongoza kikosi hicho kwenye jumla ya mechi 84 anaondoka timu ikiwa nafasi ya 9 na pointi zake kibindoni ni 29.

Inaelezwa kuwa anayetajwa kubeba mikoba ya Lampard ndani ya Chelsea ni Thomas Tuchel ambaye alikuwa kocha ndani ya Klabu ya PSG ila alifutwa kazi kutokana na matokeo mabovu.

Lampard amesema:-"Kwa muda mrefu nimekuwa ndani ya Chelsea ila ninafurahi kufanya kazi hapo,ninapenda kuwashukuru mashabiki kwa sapoti ambayo wamenipa kwa muda wa miezi 18.

"Uongozi pia na wote ambao wamekuwa pamoja nami, ninajua kwamba changamoto ni jambo ambalo haliepukiki, ila kwa kushindwa kufikia mafanikio kwangu ni maumivu, ninaushukuru uongozi kiujumla na kila mmoja, nawatakia mafanikio mema," .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic