KOCHA Mkuu wa Klabu ya Simba, Didier Gomes Da Rosa amefunguka kuwa anataka kuona kikosi chake kinatwaa makombe katika michuano yote wanayoshiriki, na kwa kuanzia wataanza na kombe la michuano ya Simba Super Cup.
Simba ilianza vizuri kibarua chake cha michuano ya Simba Super Cup baada ya kuibamiza Al Hilal ya Sudani kwa mabao 4-1 kwenye mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo iliyo na dhumuni la kuziandaa timu shiriki kuelekea michezo ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Gomez alitangazwa rasmi kuwa Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba Jumapili ya Januari 24 akichukua nafasi iliyoachwa na Mbelgiji, Sven Vandenbroeck ambaye alijiuzulu nafasi hiyo Januari 7, na kocha huyo mpya tayari amesimamia mazoezi ya kikosi chake kwa siku nne mfululizo.
Michuano ya Simba Super Cup iliyoanza jana, jANUARI 27 inashirikisha timu tatu ambazo ni Al Hilal, TP Mazembe na mwenyeji Simba.
Akizungumzia malengo ya Simba katika michuano hiyo Gomez amesema: “Kwangu kila mchezo nauchukulia kama fainali hivyo ni lazima tupambane kuhakikisha tunalichukua kombe hili.
"Hii itatujengea hali ya kujiamini na hamu ya kushinda makombe mengine katika michuano tunayoshiriki,".
Tunakusubir, wenzako walikuja na wakatoka. Hilo no kuti kavu, mkianza kupigwa hamsa za nje ndani, ndio utaelewa
ReplyDeleteUnaota ndoto za jua la saa Saba mchana,na kazi mnayo mwaka huu mnaita maji mma kombe lenu Hilo Hilo mapinduzi mliloenda kusherehekea mpaka makao makuu yenu ndilo Hilo Hilo mtajifariji Bali WEHU nyinyi
ReplyDeleteMpira sio Maneno, kwa akili yako wanaweza kuchukua kombe la club bingwa Africa?
ReplyDeleteHata hili la league wajipange sio rahisi, kwanza wamalize viporo vyao na Azam na Namungo!
Aacha kuwatoa mapovu hawa jamaa
DeleteAMUNGO NA AZAM NI TIMU ZENYE MPIRA MZURI WA KUVUTIA LAKINI WANAKOSA MKAKATI SAHIHI WAKUIPOTEZA SIMBA NDANI YA DK. 90. ANGALI KATIKA KOMBE LA MAPINDUZI, REJEA MECHI ZA MSIMU ULIOPITA KUNA KITU UTAONA HAPO. NAMUNGO YA MSIMU HUU SIO NZURI KAMA MSIMU ULIOPITA, NAJUA KUNA WATU WATAKATAA ILA WAKATI UTASEMA. SIO NAMUNGO WALA AZAM HAWAWEZI KUIFUNGA SIMBA MSIMU HUU.
Delete