January 28, 2021


 KOCHA msaidizi wa klabu ya Yanga, Nizar Khalfani amekanusha taarifa za baadhi ya watu wanaosema kuwa ana mapenzi na Simba  kwa kusema kuwa hana mapenzi yoyote na Simba kwani yeye ni shabiki wa Yanga.

Taarifa hizo zilikuwa zikipewa nguvu na kipande cha video ambayo ilikuwa ikimuonyesha Nizar akisifia uwezo wa nyota wa Simba kucheza soka la kuvutia kwenye moja ya mahojiano aliyowahi kuyafanya miaka kadhaa iliyopita.

Nizar pamoja na kocha mpya wa viungo Edem Mortotis walitambulishwa rasmi na Yanga jana Jumatano kuchukua nafasi za aliyekuwa kocha msaidizi, Juma Mwambusi na Riedoh Berdien aliyewahi kuhudumu kama kocha wa viungo na utimamu wa mwili.

Nizar na Mortotsi wamejiunga na Yanga kuimarisha benchi la ufundi kwa ajili ya kuwa na kikosi imara ambacho kitafanikisha lengo lao la kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara na kombe la FA. 

Akitolea ufafanuzi taarifa hizo Nizar amesema: "Nimekuja kuisaidia Yanga katika malengo yake ya kutwaa ubingwa msimu huu, najua kuna kipande cha video inayosambazwa mitandaoni ikinionyesha nikisifia Simba laikini napenda kuweka wazi kuwa sina mapenzi yoyote na klabu ya Simba," 

 


7 COMMENTS:

  1. Hivi uyanga na usimba ni vita mbona inakuwa zaidi hata ya dini zetu,hii kitu ifike mwisho ndo inayo dumaza soka letu la Bongo,unakuta Taifa stars imejaa siasa za Simba na Yanga mpaka inaudhi yani.

    ReplyDelete
  2. Inaonesha yanga inaivhukia sana Simba kufikia hadi hana ruhusa hata kutamka kuwa Mnyama anacheza mpira wa kueleweka. Ikiwa ana mapenzi na Simba ni wazi wa Nataka aichukie Simba lakini hawajui kuwa haiwezekani kumuamrisha mwenye akili apende hichi na akichukie kile kwasababu mapenzi yapo rohoni. Ni aibu tupu jamani viumbe hivi

    ReplyDelete
  3. Hata kama ana mapenzi hoyo ni siri yake. Kwa sasa ni kocha wa yanga mwacheni kijana wa watu apige mzigo apate malipo halali, mkimharibia atakula kwenu?

    ReplyDelete
  4. Muacheni aturahisishie kazi yetu ili tutimize malengo ya back to back for 10 years

    ReplyDelete
  5. Hao Nizari sifikiri hata kidogo kama watakuamini tena. Namkumbuka Sven wa Simba aliwahi kusifiwa uwezo wa nyota wa Yanga lakini hapana hata mmoja si viongozi wala mashabiki waliomsakama Sven kwa saba soca si uaudui lakini ni mapenzi na urafiki baina ya watu wa duniani kote lakini hapa kwetu ndio kuna viumbe wa ajabu wanaofanya mambo duniani kote hakuna. Hao waelimishwe na kupewa pole

    ReplyDelete
  6. Tabia hiyo wanayo sana simba Manula alimsifia morrison kamfunga gori zuri manara ukamponda sana acheni ushamba kusifia nikuonyesha unaukubali uwezo wa mwenzio ndoi

    ReplyDelete
  7. TUMUACHE MWANDISHI NA BLOG YAKE, KWA SABABU HAKUNA MAHOJIANO ALIYOFANYA AKATAMKA KUWA HANA MAPENZI NA SIMBA WAKATI UKOCHA NI KAZI YAKE. TUJIFUNZE ZAHERA MBWATUKAJI SANA BUT HAKUSITA KUISIFIA SIMBA KATIKA UBORA WAO WAKATI AKIWA KOCHA YANGA NA HATA LEO MKURUGENZI WA UFUNDI WA GWAMBINA.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic