January 16, 2021

 


ALIYEWAHI kuwa kocha Mkuu wa Simba Mbelgiji, Sven Vandenbroeck amefunguka kuwa hana mpango wa kumsajili mchezaji yeyote kutoka Simba wakiwemo Clatous Chama na Luis Miquissone kwenda katika timu ya Far Rabat aliyojiunga nayo hivi karibuni.


Sven hivi karibuni alijiunga na timu ya Far Rabat ya nchini Morocco mara baada ya kuondoka ndani ya Simba ikiwa ametoka kuipeleka timu hiyo katika hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika.

 

Akizungumzia ishu hiyo Sven amesema kuwa hana mpango wa kumsajili mchezaji yeyote wa Simba kwani kuna wachezaji wengi wazuri ambao anawajua wakuwasajili ndani ya timu hiyo tofauti na wale ambao wapo Simba.

 

“Nimefundisha Afrika kwa muda kidogo, nawafahamu wachezaji wengi wazuri ambao ninauhakika wakisajili hapa Far Rabat watafanya vizuri tofauti na wale ambao wanapatikana Simba, watu wanaongea kuwa nitawasajili wachezaji wa Simba lakini si ukweli kuhusu hilo.

 

“Kwa sasa mipango ni kuangalia nini nitafanya nikiwa na timu yangu mpya ili kuifanya ifanikiwe katika ligi kuu ya Morocco na wala sifikirii tena nyuma kwa kuwafuatilia wachezaji wa Simba,”

 

5 COMMENTS:

  1. Tatizo mnatunga story halafu mnakuja kukanusha ili mradi muuze magazeti

    ReplyDelete
  2. Tushawazoea mbwiga sana hawa waandishi

    ReplyDelete
  3. Hii ndo kazi yao na ndo inafanya mikono iende vinywani mwao, wewe kama msomaji wa makala za blog hii ni kuchukua taarifa ambazo ni za kweli na kuziacha ambazo unadhani si za kweli au vinginevyo ukiona wanatunga habari unaacha kuingia katika blog

    Au ukiona we unazijua habari za kweli tupe basi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic