MSHAMBULIAJI
mpya wa klabui ya Yanga, Fiston Abdoul Razak anatarajiwa kutia nchini siku ya
Alhamisi ili kujiunga na kambi ya timu hiyo inayojiandaa na michezo ya mzunguko
wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Fiston ni miongoni mwa
wachezaji watatu waliosajiliwa na Yanga katika kipindi cha dirisha dogop ambao
wanakuja kukiongezea nguvu kikosi hicho kinachopambana kushinda tajui la Ligi
Kuu msimu huu.
Kikosi cha klabu ya Yanga
kimeanza rasmi mazoezi ya kujiandaa na michezo ya mzunguko wa pili jana
Jumatatu, mazoezi yanayofanyika kwenye kambi yao ya Avic Town, Kigamboni jijini
Dar es Salaam.
Yanga inaongoza msimamo wa Ligi
Kuu Bara ambapo imejikusanyia pointi 44 katika michezo 18 waliyocheza mpaka
sasa.
0 COMMENTS:
Post a Comment