IMEELEZWA kuwa Kocha Mkuu wa Klabu ya African Lyon, inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Nizar Khalifan yupo kwenye hesabu za kupokea mikoba ya Juma Mwambusi ndani ya Yanga.
Mwambusi aliomba kuondoka ndani ya Yanga kutokana na kusumbuliwa na matatizo ya kiafya ambayo anayo kwa sasa.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga alisema kuwa Mwambusi aliandika barua ya kuomba kuondoka ndani ya Yanga kufuatia ushauri wa madaktari na aliomba kuondoka tangu wakiwa Visiwani Zanzibar.
Zanzibar kikosi kilikuwa kinashiriki Kombe la Mapinduzi ambapo walifanikiwa kutwaa taji hilo kwa ushindi wa penalti 4-3 dhidi ya Simba baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya bila kufungana.
Akizungumza na Saleh Jmebe, Khalifan amesema kuwa kwa sasa hawezi kuzungumza kuhusu kuibukia ndani ya Yanga kwa sasa.
"Nipo salama kwa sasa ila kuhusu kwenda Yanga kwa sasa Siwezi kuzungumzia jambo hilo kesho nitaweka wazi," .
0 COMMENTS:
Post a Comment