BERNARD Morrisonn kiungo mshambuliaji wa Simba ni miongoni mwa nyota ambao wameanza kufanya kazi na mrithi wa mikoba ya Sven Vandenbroeck, Didier Gomes.
Raia huyo wa Ufaransa tayari ameshaanza kazi ndani ya Uwanja wa Mo Simba Arena kwa ajili ya kukisuka kikosi hicho kwa ajili ya kuelekea michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa Simba imetinga hatua ya makundi.
Nyota wengine ambao wameanza kazi na kocha huyo ambaye amesaini dili la miaka miwili ni pamoja na:-
Thadeo Lwanga
Rally Bwalya
David Kameta
Perfect Chikwende
Miraj Athuman
Ibrahim Ajibu
Mzamiru Yassin
Kened Juma
Gadiel Michael
Chris Mugalu
Ally Salim
Mohamed Hussein
Junior Lokosa
Francis Kahata
Hassan Dilunga
Beno Kakolanya
Haya haya wachezaji wao muhimu wana matatizo na klabu? Wawa, Miquisonne, Chama wako wapi mboma taarifa haziko wazi?
ReplyDeleteWako na mapumziko
DeleteHuenda wakawepo kesho wakati wa mechi ya Simba Super Cup watakapotambulishwa rasmi
DeleteWachezaji wote wameshafika kambini isipokuwa walioƄo Chan huko Cameroon.
ReplyDelete