CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa mshambuliaji wake Yacouba Songne kwa sasa yupo fiti baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda akitibu majeraha aliyoyapata uwanjani.
Songne aliumia kwenye mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi Zanzibar dhidi ya Azam FC kwenye sare ya kufungana bao 1-1.
Alikosekana kwenye mchezo wa fainali uliochezwa Uwanja wa Amaan na kushuhudia wachezaji wenzake wakilazimisha sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90 mbele ya Simba.
Licha ya sare hiyo Yanga ilishinda kwa penalti 43 na kuwafanya wabebe Kombe la Mapinduzi mwaka 2021.
Ndani ya Ligi Kuu Bara, Yacouba ni kinara wa kutengeneza pasi za mwisho akiwa nazo nne na amefunga pia mabao manne na kumfanya ahusike kweye mabao nane kati ya 29 ambayo yamefungwa na timu hiyo.
Kuhusu hali yake Kaze amesema:-"Yacouba tayari amepona,tunatarajia ajiunge na wenzake tayari kwa mazoezi ya pamoja.
"Ni mmoja ya wachezaji wazuri ambao wanafanya vizuri wakiwa ndani ya uwanja, kuna mengi juu yake tunatarajia hivyo mashabiki wasiwe na mashaka," .
Penalti 43?
ReplyDeletehahaha dah et penalit 43
ReplyDeletehahaha dah et penalit 43
ReplyDelete