January 23, 2021


 KAMATI ya Nidhamu ya Klabu ya Simba chini ya mwenyekiti wake Suleiman Kova imetangaza hukumu ya kiungo wa klabu hiyo, Jonas Mkude ambaye alisimamishwa na uongozi kwa makosa ya utovu wa nidhamu.


Kwa mujibu wa Kova kamati hiyo imempa masaa 24 kiungo huyo kuomba msamaha kwa maandishi huku ikiweka hadhari makosa ambayo yalisababisha nyota huyo kusimamishwa Desemba 28,2020.

Haya ndiyo makosa aliyokuwa akituhumiwa kuyafanya, pamoja na hukumu zake.

Moja: Kutohudhuria semina elekezi iliyohusisha wachezaji, benchi la ufundi na viongozi. Adhabu yake ni faini ya shilingi milioni moja (1,000,000).

Mbili: Kuchelewa kuingia kambini wakati timu ilipokuwa ikijiandaa na mchezo dhidi ya Coastal Union. Adhabu aliyopewa ni karipio kali na faini ya shilingi milioni moja (1,000,000) na kuwekwa katika kipindi cha uangalizi cha miezi sita.

Tatu: Kutoripoti kambini siku ya 26/11/2020 bila ruhusa. Katika tuhuma hizi, kamati haikumkuta na hatia baada ya kamati kutothibitisha pasipo shaka shitaka hilo.

Pia Kamati ya Nidhamu imemtaka Mkude kurejea kambini mara moja kuendelea na mazoezi na asipofanya hivyo atakuwa amefanya tena kosa la utovu wa nidhamu.

Faini aliyotozwa anatakiwa kuilipa ndani ya mwezi mmoja.

Kamati imemtaka Mkude kuomba radhi kwa maandishi ndani ya saa 24.
Tayari Mkude aliomba radhi kwa njia ya sauti kwa mashabiki wa Simba kwa kitendo ambacho alikifanya na kuomba msamaha huku akiahidi kwamba hatarudia tena.

Wakati wa hukumu yake ikisisikilizwa na kamati ya nidhamu alikosekana kwenye jumla ya mechi saba ambapo nne zilikuwa ni za Kombe la Mapinduzi, Visiwani Zanzibar na moja ya Kombe la Shirikisho, moja ya Ligi Kuu Bara na moja ilikuwa ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

2 COMMENTS:

  1. Kama hayo hayatokuweka sawa basi umekwisha na sifa ulizkuwa nazo zitachukuliwa na. pepo na jina lako litabakia kukumbukwa katika waliojimaliza wenyewe

    ReplyDelete
  2. Huwezi kuwa mkubwa mbele za watu, hata kama ww nimkubwa kiumri n.k
    ukifanya hovyo utashushwa tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic