HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar amesema kuwa anaamini mzunguko wa pili utakuwa na ushindani mkubwa jambo ambalo linamfanya afikirie mbinu mpya za kupata matokeo chanya.
Mtibwa msimu wa 2020/21 haujawa mzuri kwake licha ya kubadilisha kocha kwa kuwa Zuber Katwila alibwaga manyana na kwa sasa yupo zake ndani ya Ihefu FC akipambania kombe.
Ikiwa imecheza jumla ya mechi 18 imejikusanyia jumla ya pointi 22 ikiwa nafasi ya 11 huku Ihefu ya kocha wao wa zamani ikiwa nafasi ya 18 na imecheza mechi 18 kibindoni ina pointi 13.
Aliibuka ndani ya Mtibwa Sugar baada ya kupewa mkono wa kwa heri ndani ya Namungo FC ambayo kwa sasa inanolewa na Kocha Mkuu, Hemed Morroco.
Akizungumza na Saleh Jembe, Hitimana amesema kuwa kuna kazi kubwa ya kufanya kwenye mzunguko wa pili ili kuwa imara.
"Naona kuko na kazi kubwa ya kufanya mzunguko wa pili hasa ukizingatia kwamba kila timu inahitaji ushindi na ni wakati wa kila mmoja kujua wapi atakuwa.
"Kweli ushindani ni mkubwa hilo lipo wazi ila ninaamini kwamba mbinu mpya zitafanya kikosi kipate matokeo mazuri bado tuna nafasi ya kufanya vizuri," .
0 COMMENTS:
Post a Comment