IMEELEZWA kuwa Uongozi wa Simba upo kwenye hesabu za kuinasa saini ya kipa namba moja wa Biashara United, Daniel Mgore ili kumpa changamoto mpya kipa wao namba moja Aishi Manula.
Mgore anatajwa kuingia pia kwenye anga za Azam FC ambapo aliweka wazi kwamba amefuatwa na mabosi wa timu hiyo wakimuulizia mkataba wake.
Habari kutoka ndani ya Simba zimeeleza kuwa tayari mabosi hao ambao wapo kwenye Kombe la Mapinduzi na jana waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Chipukizi wameanza hesabu za kuinasa saini ya nyota huyo.
"Mpango mkubwa ni kumpata kipa mmoja ambapo awali alikuwa anahitajika kipa kutoka nje ya nchi ila kwa namna ambavyo kuna vijana wenye uwezo basi anaweza kuchukuliwa yule Mgore,(Daniel) wa Biashara United," ilieleza taarifa hiyo.
Barbara Gonzale, Mtendaji Mkuu wa Simba kuhusu suala la usajili amesema kuwa bado kuna wachezaji ambao wanawatazama na ikiwa wataweza kufikia vigezo basi watasajili.
Kama sielewi vile. Hivi hii biashara ina mpango wa kuiza timu nzima?
ReplyDelete