NYOTA wa zamani wa Klabu ya Tottenham Hotspur, inayonolewa na Kocha Mkuu, Jose Mourinho amegomea dili la kurejea ndani ya timu hiyo msimu ujao.
Christian Eriksen alikuwa ndani ya Spurs na aliuzwa ndani ya Klabu ya Inter Milan na huko kwake mambo yamekuwa magumu kwa kuwa hajaweza kuwika.
Taarifa zimekuwa zikieleza kuwa Spurs inahitaji kumrudisha kiungo huyo kikosini ili aweze kuendelea kupambania ndoto zake za kuwa nyota wa kimataifa.
Habari zimeeleza kuwa kiungo huyo amegoma kurejea ndani ya timu hiyo kwa kuwa anaamini kwamba anaweza kupata nafasi ndani ya Inter Milan na kuwika upya.
Mbali na Spurs nyingine ambazo zinatajwa kuwania saini yake ni Wolves,Arsenal na Real Madrid.
0 COMMENTS:
Post a Comment