January 18, 2021


 SELEMAN Matola, Kaimu Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba amesema kuwa kilichowafanya wapoteze kwenye mchezo wao wa fainali dhidi ya watani zao wa jadi Yanga ni matokeo ya mpira ndani ya uwanja.

Simba kwenye Kombe la Mapinduzi ilitinga hatua ya fainali kwa kushinda mechi zake zote tatu ila ilikwama kusepa na taji la Mapinduzi baada ya kushindwa kuwafunga watani zao wa jadi Yanga.

Fainali hiyo iliyochezwa visiwani Zanzibar, Uwanja wa Amaan, dakika 90 zilikamilika kwa sare ya bila kufunga ila kwenye mikwaju ya penalti Simba ilikosa penalti mbili zilizopigwa na Meddie Kagere na Joash Onyango.

Kwa upande wa Yanga ni penalti moja ilikoswa iliyopigwa na Tonombe Mukoko na kufanya Yanga ishinde kwa mabao 4-3.

Akizungumza na Saleh Jembe, Matola amesema kuwa kilichotokea Uwanja wa Amaan ilikuwa ni sehemu ya matokeo ya mpira jambo ambalo hawawezi kulibadilisha.

"Wachezaji walipambana ndani ya uwanja kusaka matokeo ila haikuwa bahati yetu kuweza kutwaa ubingwa hivyo hakuna chaguo.

"Kwa kilichotokea ni maumivu lakini ikumbukwe zile zilikuwa penalti na hakuna fundi linapofika suala la penati hakuna namna ya kubadilisha," amesema.

Yanga inakuwa imefikisha jumla ya mataji mawili ya Kombe la Mapinduzi huku Simba ikiwa na mataji mawili ya Kombe la Mapinduzi.

5 COMMENTS:

  1. Hiyo siyo sababu ya kutolewa na MTAALAMU otherwise umetunga wewe,

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sababu kubwa ni ukwrli kuwa penalti hazina mwenyewe. Timu zilitoshana nguvu ndani ya dakika 90

      Delete
  2. wakubali tu kuwa walizidiwa tu mpira maana hata short on target ilikuwa 5-0

    ReplyDelete
  3. Short on target zote hizo halafu zero goals!!! Duh

    ReplyDelete
  4. Wewe hata Jana Liver na Man U walitoka 0-0 huwezi sikia sababu za Kocha asiyejua kueleza kilichotokea Uwanjani Kama huyu ,mfano Kocha wa Man u anasema hatukustaili kushinda sababu ni kwamba tulikuwa hatupo vizuri kumiliki mpira tuliupoteza Sana ,ingawa kipindi Cha pili tulibadilika japo si Sana na kidogo tupate goli kwani tulitengeneza nafasi Kama mbili za kupata goli,Sasa huyo Kihiyo wenu Zama hizi eti matokeo Uwanjani tulipambana na mpira una matokeo matatu na Penalty hazina mwenyewe hayo ndiyo maelezo ya kilichotokea Uwanjani dk 90 kwa mujibu wake.Halafu upuuzi zaidi eti kapelekwa kuongeza nguvu Morocco hongera TFF .Kocha alikuwa na Bench lenye Wachezaji wazuri akashindwa kulitumia dhidi ya Timu ambayo benchi lilikuwa na makipa wawili Yanga B watatu na senior players wawili AMBAO nao kuingia kwao ilikuwa Kama gamble hususan Waziri Junior,Paul Godfrey ni baada ya kuumia Adeyum.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic