January 28, 2021




 CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga amesema kuwa ataanza kuwaweka sawa kisaikolojia wachezaji wake ambao ameanza nao mazoezi ikiwa ni pamoja na Tuisila Kisinda na Lamine Moro.

Kisinda ambaye msingi wake namba moja ni mbio amehusika kwenye mabao manne ndani ya Yanga akiwa amefunga mabao mawili na kutoa pasi mbili za mabao huku Lamine akiwa ni kinara kwa watupiaji kwa mabeki Bongo akiwa amefunga mabao manne na pasi moja ya bao.

Tayari kikosi kimeanza mazoezi Januari 25 ikiwa ni kwa ajili ya maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara zinazotarajiwa kurejea Februari 13 pamoja na Kombe la Shirikisho ambapo Yanga imetinga hatua ya 32 bora.

Kaze amesema:”Kazi kubwa kwa sasa ni kuirejesha saikolojia ya wachezaji wangu katika hali yao ya kawaida hasa baada ya mapumziko mafupi ambayo walikuwa wameyapata na kuwapa majukumu mapya.

"Ninaona kwamba wachezaji wanazidi kurejea kwenye ubora ila haitakuwa kwa haraka lazima waanze taratibu kabla ya kurejea kwenye ule ubora ambao wamekuwa nao awali," . 

Miongoni mwa wachezaji ambao wameanza mazoezi ni pamoja na Paul Godfrey, Tonombe Mukoko, Carlos Carilnhos, Wazir Junior.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic