BERNARD Morrison amesema kuwa atazidi kufanya vizuri ndani ya kikosi chake cha Simba licha ya wengi kueleza kuwa ana hernia jambo ambalo halina ukweli.
Jana, Januari 27 Uwanja wa Mkapa wakati Simba ikishinda kwa mabao 4-1 dhidi ya Al Hilal kwenye mchezo wa Simba Super Cup, Morison aliweza kubadili mchezo ndani ya dakika 27 ambazo alitumia.
Aliingia akitoka benchi dakika ya 63 akichukua nafasi ya Francis Kahata ambapo aliweza kutumia dakika nane kuonyesha makeke yake kabla ya bao la pili kufungwa.
Shuti lake lililolenga lango dakika ya 71 lilikutana na mikono ya kipa wa Al Hilal ambaye aliokoa shuti hilo kisha Perfect Chikwende alikutana nalo na kufunga bao la pili kwa Simba na likiwa ni la kwanza kwake msimu wa 2020/21 kwa kuwa amejiunga na Simba akitokea Klabu ya FC Platinum ya Zimbabwe.
Dakika ya 86 Morrison alipachika bao la tatu likiwa ni la kwanza kwake na dakika ya 89 alipachika bao la nne na la pili kwake na dakika ya 90+4 alionyeshwa kadi ya njano ikiwa ni ya kwanza kutolewa kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.
Morrison amesema :"Naskia kwamba wanasema nina hernia sawa kwa kuwa wanasema ninayo nami ninawaonyesha kile ambacho nimepewa ndani ya uwanja.
"Furaha yangu ni kuona mashabiki wanapata matokeo nami pia nitazidi kupambana kila ninapopata nafasi kufanya kazi kweli kwani hakuna namna ambayo ninaweza kufanya zaidi ya kucheza ndani ya uwanja," .
Kesho Simba Super Cup itaendelea ambapo Al Hilal itakuwa na kibarua cha kusaka ushindi mbele ya TP Mazembe anayocheza Mtanzania, Thomas Ulimwengu.
Waonyeshe hao wanaokubeza kwa vitendo *watakereka sana msimu huu.
ReplyDelete