BALAMA Mapinduzi, kiungo mshambuliaji ndani ya kikosi cha Yanga kwa sasa yupo nchini Tanzania akiendelea kuwa chini ya uangalizi baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti nchini Afrika Kusini.
Balama alipata maumivu hayo kwenye mazoezi ya timu yake msimu uliopita na amefanyiwa upasuaji mara mbili ili kuweza kurejea kwenye ubora wake.
Alirejea kutoka Afrika Kusini, Januari 21, matibabu aliyofanyiwa awali hapa Bongo yalishindwa kumrejesha kwenye ubora wake kiungo huyo kipenzi cha Wanajangwani.
Anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki tano huku akitazamiwa afya yake ikiwa atakuwa fiti ili arejee uwanjani kuanza na programu ya mazoezi.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa kurejea kwake ni furaha kwa timu kwa kuwa wanaamini kwamba atarejea kuendelea kupambana.
"Tuna amini kwamba kurejea kwake ni sehemu ya mafanikio na akirejea kwenye ubora wake ataendelea na majukumu yake kama zamani hilo ni jambo ambalo tunalitarajia.
"Kwa sasa ataendelea kuwa chini ya uangalizi mpaka baada ya wiki tano hapo kutakuwa na taarifa mpya ambazo zinaweza kutolewa kuhusu afya yake," .
Mlimchelewesha kumpeleka SA
ReplyDelete