IMERIPOTIWA kuwa Klabu ya Liverpool ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England imemalizana na beki wa kati wa Klabu ya New York Red Bulls, Aaron Long.
Hatua hiyo imefikia baada ya Liverpool kutokuwa imara upande wa ulinzi kutokana na mabeki wake wengi kuwa ni majeruhi ikiwa ni pamoja na Virgil van Dijk ambaye ni beki kisiki wa kati na Joe Gomez hawa wanatarajiwa kukaa nje msimu mzima wakitibu majeraha yao.
Pia Joel Matip aliumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Tottenham hivyo naye anasumbuliwa na majeraha jambo ambalo linawafanya Liverpool wasiwe na chaguo zaidi ya kuhitaji saini ya beki huyo mwenye miaka 28 kwa mkopo.
Jurgen Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool amesema kuwa watafanya jitihada ili kuweza kuwa imara katika safu ya ushambuliaji pamoja na ulinzi ambavyo vyote vinategemeana ndani ya uwanja.
"Kila kitu ndani ya uwanja kinategemeana, ninaskia kwamba wanasema nisajili beki wa kati sasa hapo unaweza kujiuliza nikipata beki nitakuwa nimemaliza matatizo yote ndani ya timu? Bado tuna kazi ya kufanya na kila kitu kinawezekana licha ya kwamba kwa sasa tupo kwenye wakati mgumu," .
Klopp asijifanye kichwa ngumu, hana mabeki, forward kunatosha
ReplyDelete