BARAZA la Michezo Tanzania (BMT), leo linatarajiwa kusimamia uchaguzi mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania (RT).
Uchaguzi huo ni wa kikatiba na unatarajiwa kujaza nafasi
mbalimbali za uongozi katika chama hicho.
Akizungumzia kuhusu uchaguzi huo, Katibu Mkuu wa RT, Ombeni Mzavara amesema: “Maandalizi yote ya
uchaguzi mkuu wa chama cha riadha Tanzania yamekamilika.
“Kwa mwaka huu tunatarajia uchaguzi huu utasimamiwa na BMT, ambao
wamehusishwa katika mchakato mzima wa uchaguzi tangu utaratibu wa kuchukua na
kurudisha fomu,”
0 COMMENTS:
Post a Comment