UONGOZI wa Simba umeshikwa na kigugumizi cha kuweka ukweli juu ya hatma ya kiungo mshambuliaji, Francis Kahata ndani ya kikosi hicho kilicho chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Seleman Matola.
Kahata maisha yake ndani ya Simba msimu wa 2020/21 yamekuwa yake peke yake kwa kuwa hana nafasi kikosi cha kwanza kutokana na ushindani wa namba.
Alianza kupewa nafasi ya kudumu kwenye Kombe la Mapinduzi baada ya Sven Vandenbroeck kubwaga manyanga Januari 7 kwa kile alichoeleza kuwa ni matatizo ya kifamilia ila kwa sasa yupo nchini Morroco akikinoa kikosi cha FAR Rabat.
Imekuwa ikielezwa kuwa kiungo huyo muda wake ndani ya Simba umekwisha ambapo mabosi walitaka kumtoa kwa mkopo kwenda Azam FC ila Kahata akagomea dili hilo jambo ambalo limeongeza presha ya kuachana naye msimu utakapoisha.
Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa Kahata ni mchezaji wa Simba ila itafahamika hivi karibuni.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa hawawezi kujadili ishu ya mchezaji mmoja kwa kuwa wana mambo makubwa wanataka kufanya.
"Simba ni timu kubwa,tunawaza makubwa kuhusu Simba Super Cup unaanza kuleta habari nyingine, hakuna siasa ila kazi,tutazungumza baadaye," .
Kahata amesema:"Sijui kuhusu kuachwa ama kutolewa kwa mkopo mimi ni mchezaji wa Simba,".
0 COMMENTS:
Post a Comment