UONGOZI wa Yanga umesema kuwa kwa sasa kalenda mpya za Yanga zinapatikana makao makuu ya Klabu ya Yanga pamoja na maduka yote ya GSM ambao ni wadhamini pia wa timu hiyo hivyo mwanachama anatakiwa kutamba na kalenda hiyo .
Yanga inanolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze ipo nafasi ya kwanza Kwenye msimamo na pointi zake ni 44 baada ya kucheza mechi 18.
Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa kalenda hiyo mpya ina matukio yote muhimu yanayohusu timu hiyo kuanzia Kwenye suala la upokeaji wa rasimu.
"Kalenda ipo tayari,mwanachama ni wajibu wako kutamba na kuvimba na kalenda baada ya kujipatia Malala yako kwa kuwa ni mali ya Yanga na ina ubora wa hali ya juu.
"Kuna matukio muhimu ambayo yapo ndani ya kalenda ikiwa ni pamoja na siku ya makabidhiano ya rasimu pamoja na picha zenye ubora kabisa hivyo ni wajibu wako kutamba," .
Bei ya kalenda mpya ndani ya mwaka mpya 2021 ni buku tano tu.
Mhpfeeeew kalenda
ReplyDeleteNi staili nyinyine ya kutembeza makopo ya kuombea
Inaelekea ukipewa uganga ukairoge yanga, uko radhi,
Delete