January 15, 2021


 UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa nyota wa wawili watakuwa sehemu ya kikosi ambacho kimeweka kambi Visiwani Zanzibar kwa muda wa siku 10 ikiwa ni kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu Bara.

Nyota hao ni pamoja na mshambuliaji wao namba moja Prince Dube ambaye alikuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki sita kutokana na kuumia mkono wa kushoto.

Ndani ya Ligi Kuu Bara, Dube ametupia mabao sita na ana pasi nne za mabao akiwa ni namba moja ndani ya Azam FC.

Pia nyota mwingine ambaye ameanza mazoezi ni kipa wao mpya Mathias Kigonya ambaye amesaini dili la miaka miwili kutumika ndani ya Azam FC.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa wakiwa visiwani Zanzibar watacheza michezo ya kirafiki ili kuwa bora.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic