IMEELEZWA kuwa Bernard Morrison nyota wa kikosi cha Simba atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi sita kutokana na matatizo ya kiafya.
Nyota huyo amekuwa hana nafasi ndani ya kikosi cha Simba baada ya kuibukia huko akitokea Klabu ya Yanga ambayo imekuwa ikieleza kuwa bado mchezaji huyo ni mali yao.
Kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi uliochezwa Uwanja wa Amaan, Januari 13 dhidi ya Yanga alikuwa benchi na alipata muda wa kufanya mazoezi ila hakuingia kucheza.
Timu yake ilipoteza kwa kufungwa penalti 4-3 baada ya dakika 90 kukamilika kwa sara ya bila kufungana kwa watani hao wa jadi na kufanya ubingwa uende mitaa ya Jangwani.
Taarifa iliyotolewa na Kassim Dewji, Mjumbe wa Bodi ndani ya Simba imeeleza kuwa:"Mchezaji Morrison anaumwa na imeshauriwa aweze kufanyiwa vipimo zaidi ili aweze kurejea ndani ya uwanja.
"Kwa muda mrefu hajawa uwanjani na amekuwa hafanyi mazoezi na wenzake zaidi ya mazoezi mepesi kuna programu ambayo amepewa hivyo mpaka afanyiwe upasuaji atarejea ndani ya uwanja.
"Hajaonekana kwa muda mrefu akicheza hilo lipo wazi na imeshauriwa kuwa akae nje ya uwanja kwa muda wa miezi sita ndipo atarejea kwenye ubora wake," ilieleza taarifa hiyo.
SEMENI TU MNASUBIRI ISSUE YAKE NA YANGA IISHE ILI MSIINGIE HASARA KUPOKWA POINTS...
ReplyDeleteHAIWEZEHKANI MTU AWE SEHEMU YA KIKOSI KAMA ALIKUWA MGONJWA ANGEBAKI DAR KABISA. SIMBA IMEINGIA CHA KIKE KWENYE USAJILI WA HUYU JAMAA. HUU NDIO USAJILI HEWA ANAOITA MANARA.
SASA KAMA ANAUMWA WALITAKA WAKWAMBIE MZIMA? SIMBA HAINA MCHEZA MMOJA ACHA AKAE TU
DeleteKweli ukitoka Yanga kwa mbwembwe mwendo hamna
ReplyDeleteMorrison kutocheza simba haipungizii kitu kwani lengo ilikuwa ni kumuondosha Yanga baSi kazi imekwisha. Tunawaomba Yanga kuwa wastaarabu la sivyo tutawaliza tena ili waendelee kuhangaike na CAS.
ReplyDeleteNa utopolo wakiendelea kuchonga tunamuondoa mwingine asicheze kwao na kwetu, halafu tunaendelea kumlipa
ReplyDeleteDishi limeyumba huyo jamaa mpelekeni Mirembe.Hanna upasuaji hapo mnatuzuga tu, kwenye mechi ya fainali ya mapinduzi cup dishi lilikuwa linataka kuanguka kabisa.Hivyo ndio Mana hata mechi yenyewe hakucheza. Alikuwa anaangaika Kama vile kuku anataka kutaga ������.
ReplyDeleteYanga Ushirikina wa nini juu ya Morrison.Mchezaji mwenyewe kaamua kuondoka kwanini mnahangaika kumdhuru ili ashindwe kutimiza ndoto zake.Waswaahili wanasema mfanyia mabaya mwenzake anaasili ya ubaya na ipo siku utamla mwenyewe.
ReplyDeleteSimba, tulieni muendelee kukerwaaaaaa
ReplyDeleteMi nafikiri nyie ndio mnaokereka na Simba na ndio Mana kombe la mapinduzi mmeshangilia Kama mmechukua UEFA champions league Tena kwa penalti,halafu kikosi Cha pili,Simba tunawaza Mambo makubwa Caf champions league ufananishe na nyie matahira fc
Delete