MAJERAHA ya nyama za paja
aliyoyapata kiungo mshambuliaji nyota wa Klabu ya Yanga, Yacouba Sogne
yameendelea kukiweka kikosi hicho katika hofu kubwa ya kumkosa nyota huyo kwa
muda mrefu.
Yacouba aliyehusika kwenye mabao
nane ya Yanga akifunga mabao manne na kuasisti mara nne alipata majeraha hayo
kwenye mchezo wa nusu fainali ya kombe la Mapinduzi dhidi ya Azam na kumfanya
akosekana kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Simba uliopigwa siku ya Jumatano, Januari 13.
Kwenye fainali hiyo Yanga
waliibuka mabingwa baada ya kuifunga Simba kwa mikwaju ya Penalti 4-3 walitwaa
taji hilo kwa mara ya pili tangu kuanzishwa kwa kombe hilo rasmi mwaka 2007.
Akizungumzia hali ya Yacouba,
Meneja wa kikosi cha Yanga Hafidh Saleh amesema nyota huyo bado anasumbuliwa na
maumivu ya nyama za paja na anatarajiwa kufanyiwa vipimo tena ili kujiridhisha
juu ya hali yake.
“Yacouba bado anasumbuliwa na majeraha ya
nyama za paja, hapo mwanzo tulitarajia angekuwa sehemu ya mchezo wa fainali
dhidi ya Simba siku ya Jumatano lakini kwa bahati mbaya haikuwa hivyo.
“Hii ni baada ya madaktari kuamuru aendelee
kupata mapumziko na atafanyiwa tena vipimo ili kujiridhisha juu ya maendeleo
yake,”
Kuhusu safari ya kurejea kwao
jijini Dar es Salaam Saleh alisema: “Kikosi chetu kipo safarini kurejea jijini
Dar es Salaam leo Ijumaa ambapo taratibu nyingine za mapumziko
zitafuata, kabla ya kurejea kambini,”.
Daaah nyama za paja zinasumbua Sana, Kama vipi afanyiwe upasuaji mapema
ReplyDeleteMtibun halaka ajiuge nawezie watimize malengo walio jiwekea kwenye timu
ReplyDeleteDah Mungu amjalie apone haraka ili arudi kwendelea na harakati za kusaka ubingwa
ReplyDeleteMungu amsaidie apone
ReplyDelete