BAADA ya kutupia bao moja akiwa na jezi ya klabu ya Azam katika michuano ya kombe la Mapinduzi, straika mpya wa klabu hiyo raia wa DR Congo, Mpiana Monzinzi amefunguka kuwa atafunga sana ndani ya kikosi hicho.
Monzinzi alikamilisha rasmi
usajili wake ndani ya Azam Desemba 23, mwaka jana akisaini mkataba wa
mwaka mmoja kutokea kikosi cha FC Lupopo, amekuja kuchukua nafasi ya Mcameroon
Alain Thierry Akono Akono aliyeuzwa nchini Malaysia.
Akizungumzia matarajio yake ndani ya kikosi cha Azam, Monzizi amesema: “Nashukuru kwa kuanza vizuri nikiwa na kikosi cha Azam, ambapo nimefunga bao kwenye mchezo wangu wa awali ambalo limeongeza ari yangu.
“Nimekuja hapa kusaka changamoto
mpya nikijua wazi kwamba soka la Tanzania lina ushindani mkubwa, na nimejiandaa
kufanya makubwa kwa kufunga mabao mengi ili kuisaidia timu yangu,” alisema
Monzinzi.
0 COMMENTS:
Post a Comment