January 16, 2021


 UONGOZI wa Klabu ya Majimaji umesema kuwa malengo yao makubwa kwa msimu huu wa 2020/21 ni kuweza kurejea ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2021/22.

Timu hiyo ilitolewa na Simba kwenye Kombe la Shirikisho kwa kufungwa mabao 5-0, Uwanja wa Mkapa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Meneja wa Klabu ya Majimaji, Godfrey Mvula amesema kuwa wanatambua kwamba wamekosa Kombe la Shirikisho ambalo ilikuwa njia kwao kupeperusha bendera kimataifa watawekeza nguvu kwenye Ligi Daraja la Kwanza.

"Kwa sasa nguvu kubwa ipo kwenye Ligi Daraja la Kwanza ambapo tunahitaji kufanya vizuri ili kurudi kwenye ushindani kama livyokuwa zamani.

"Jukumu letu viongozi ni kusimamia mambo yaliyopo yaweze kwenda sawa huku tukiomba sapoti ya mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kila saa kila wakati," amesema.

Ndani ya Ligi Kuu Bara kilishuka msimu wa 2017/18 na kwa sasa kinapambana ndani ya Ligi Daraja la Kwanza.

1 COMMENTS:

  1. Pambaneni wanalizombe. Rudisheni enzi za Selestini Sikinde, Samli Ayubu; Juma mhina, Abdallah Mrope. Hiyo ndio Icony ya Songea. Shime Mkuu wa Mkoa na Wabunge mhenzini Lawrence Mutazama Gama aliyehamasisha ujenzi wa Uwanja wa Majimaji na kuanzisha timu. Sisi ni wasomi zaidi kuliko akina Marehemu Gama tujitahidi na sisi tuache Legacy kwa kizazi kijacho.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic