January 16, 2021




IVAN Jacky Minnaert raia wa Ubelgiji ni mmoja kati ya makocha waliofanya mazungumzo na uongozi wa Simba kwa ajili ya kuchukua mikoba ya Sven Vandenbroeck raia wa Ubelgiji.

Tayari majina ya makocha Rene Weiler raia wa Uswis ambaye ni kocha wa zamani wa Al Ahly, Frolent Ibenge wa DR Congo na Hicham Aboucheroune wamekuwa wakihusishwa na kuwepo katika mpango lakini suala la mishahara yao mikubwa imekuwa kikwazo cha timu hiyo.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya bodi ya wakurugenzi wa Simba zinadai kuwa uongozi wa timu hiyo umefanya mazungumzo ya siri na Mbelgiji huyo kwa lengo la kutaka kumpa kazi ya kuionoa timu hiyo.

Uongozi wa Simba umekubaliana kutafuta kocha wa kawaida lakini ambaye wanaamini atakuwa na uwezo mkubwa katika timu hiyo ambapo wamefikia kufanya mazungumzo na kocha huyo anayeifundisha Al-Ittihad Tripoly   inayoshiriki Ligi ya Libya.

Mtu wa  karibu wa kocha huyo amesema: “Ni  kweli Simba wamefanya mazungumzo na Ivan lakini bado hawajafikia pazuri ingawa bado wanaongea,” alisema mtoa taarifa.

Ivan Minnaert ni nani?

Minnaert ni kocha wa Ubelgiji mwenye leseni ya Shirikisho la Soka Ulaya ‘UEFA Pro’ aliyotolewa mwaka 2012 na  Chama cha Soka cha Hispania.

Kocha huyo amewahi kuifundisha Djoliba AC  ya Mali mwaka 2014 kabla ya mwaka 2016 kujiunga na AFC Leopards ya Kenya kisha mwaka 2017 alijiunga AS Kaloum Star ya Guinea akichukua mikoba ya Adda Benamar.

Lakini mwishoni mwa mwaka 2017 aliitwa katika kikosi cha Black Leopards ya Afrika Kusini kudumu katika nafasi ya usaidizi chini ya Jean-François Losciuto kabla mwaka huo ukuchukuliwa na Mukura Victory ya Rwanda kwa mkataba wa miezi sita na baadaye akajiunga Rayon Sport ya Rwanda.


Mafanikio  CAF


Kocha huyo akiwa na Rayon Sport alifanikiwa kuipeleka katika hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho kutoka  katika kundi moja na Yanga USM Alger na Gor Mahia ya Kenya.

Yanga wanamkumbuka kocha huyo baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 katika mchezo wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho kwa msimu wa mwaka 2018 baada ya kutoka sare katika mechi ya kwanza iliopigwa jijini Dar.

6 COMMENTS:

  1. Ongezeni dau aje Ibenge. Kocha bora ataleta mbinu bora na mafanikio makubwa. Ibenge analijua soka la africa na n kocha wa mbinu nyngi

    ReplyDelete
    Replies
    1. TATIZO LA IBENGE ANA MKATABA NA AS VITA,PIA NI KOCHA WA TIMU WA TAIFA. UNADHANI ATAFANYA KAZI NGAPI?

      Delete
  2. Nadhani simba wajiongeze zaidi kwenye kuleta kocha mshindani zaidi. Labda kwa ushauri tu kama ujumbe utafika viongozi wa simba watafute kocha mwenye uwezo wa kuzicheza mechi za timu za Africa kaskazini kwa mafanikio zaidi.Ndio maana Elmerekh ya Sudan wanakocha wa zamami wa zamaleki au ismailia kama sikosei. Almerekh ni moja ya timu mtego zaidi kwenye kundi la simba wanatakiwa kuwa makini.

    ReplyDelete
  3. Wakikwepa gharama lazima wapate kocha wa chini ya kiwango

    ReplyDelete
  4. Kwani sveni alikiwa anajulikana cha msingi ni kumwamini mtu

    ReplyDelete
  5. Tunataka anayewajua vizuri Waarabu na mbinu zao, hapo tutatoboa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic