January 24, 2021


 UONGOZI wa Mbeya City umesema kuwa una matumaini ya kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara baada ya kufanya usajili makini pamoja na maboresho katika sehemu ambazo zilikuwa zina makosa.

Miongoni mwa nyota ambao wamesajiliwa ndani ya kikosi hicho chenye maskani yake Mbeya huku kikitumia Uwanja wa Sokoine kwenye mechi zake za nyumbani ni pamoja na beki David Mwasa.

Mbali na Mwasa yupo pia kipa mkongwe Ali Mustapha maarufu kama Batezi, ambaye ataungana na kipa mwenzake, Haroun Mandada ambaye ni kipa namba moja, Jamal Mwambeleko, Touya Didier na Juma Luzio.

Ofisa Habari wa Mbeya City, Shaha Mjanja amesema kuwa mipango ipo sawa hasa baada ya kuboresha kikosi hicho kwenye dirisha dogo.

"Kila kitu kinakwenda sawa na baada ya kukamilisha usajili kwa sasa tupo na kazi ya kupambana kwa ajili ya mzunguko wa pili.

"Kikubwa ni kwamba tunajua kwamba mzunguko wa pili ni wakati wa kusaka pointi za ushindi na malengo yetu ni kuona kwamba tunabaki ndani ya Ligi Kuu Bara, mashabiki wazidi kutupa sapoti," .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic