January 24, 2021


 MECKY Maxime, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amesema kuwa anaamini wachezaji wake watafanya kazi kubwa mzunguko wa pili kwa kupiga kazi uwanjani na kutoa burudani.

Kagera Sugar imecheza jumla ya mechi 18 ipo nafasi ya nane kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Imekusanya pointi 22 safu yake ya ushambuliaji inayoongozwa na Yusufu Mhilu ambaye yupo Cameroon kwenye kikosi cha timu ya Taifa kinachoshiriki michuano ya Chan imetupia jumla ya mabao 18.

Akizungumza na Saleh Jembe, Maxime amesema kuwa anatambua mzunguko wa pili utakuwa na ushindani ila watapambana kufanya vizuri.

"Ni muda wa wachezaji wangu kuendelea kupambana na kutoa burudani kwa mashabiki ambao watajitokeza ndani ya uwanja hata wale ambao watakuwa wanatufuatilia nje ya uwanja.

"Ninachoweza kusema ni kwamba mashabiki waje uwanjani kisha waone burudani kwani tupo imara na tupo tayari kwa ushindani," .

Kinara wa Ligi Kuu Bara ni Yanga kibindoni ana jumla ya pointi 44 baada ya kucheza jumla ya mechi 18.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic