January 20, 2021

 

 

Kampuni inayojihusisha na Mchezo wa kubahatisha ya Meridian Bet imetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa walemavu wanaosali katika kanisa la Waadiventista wasabato Mansese Jijini Dar es Salaam



Akizungumza wakati akitoa msaada huo Meneja Ustawi wa Kampuni hiyo Amani Maeda  amesema Kampuni hiyo imejiwekea utaratibu wa kusaidia watu wenye uhitaji maalum ambapo leo wameamua kutoa msaada kwa taasisi hii.

"Huu ni muendelezo wa kutoa msaada kwa watu wenye uhitaji maalum na hapa tumekuja na Mchele, unga wa ugali, sukari, mafuta ya kupikia, pempas za wakubwa pamoja na miwani lakini mtatuambia changamoto mlizonazo ili kwenye mkono wa kugusa Jamii tuweze kuwafikia" Alisema Amani Maeda.



Kwa upande wake Mratibu wa walemavu hao Oloo Vincent ameshukuru kwa msaada huo ambapo pia ametumia nafasi hiyo kuiomba Serikali pamoja na Jamii kwa ujumla kuwaunga mkono walemavu hao kwa wanachokifanya kwani pamoja na ulemavu walionao lakini wanaji shughulisha na ushonaji wa viatu.

Nae Mwenyekiti wa walemavu hao  Isdori Mrisho ameishukuru Kampuni hiyo kwa moyo wao wa utoaji na kuongeza  kuwa  watu wengi wanauwezo mzuri kiuchumi lakini hawana moyo wa utoaji.



Akizungumza kuhusiana na kuwakumbuka walemavu walioko vijijini Katibu wa Walemavu hao Berdina Sailas amesema kuwa asilimia kubwa ya walemavu wako vijijini na hawapati msaada kwa kuwa watu hawawafikii hivyo ameiomba Kampuni ya Meridian Bet iangalie namna ya kuwafikia walemavu walioko vijijini.

4 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic