January 20, 2021

 


MSHAMBULIAJI wa zamani wa Klabu ya Yanga, Amiss Tambwe amesema kuwa usajili wa nyota mpya, Fiston Abdurazak utaiongezea makali safu ya ushambuliaji ambayo ilikuwa na tatizo la umaliziaji wa nafasi za kufunga.

Kwenye usajili wa dirisha dogo Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze imemalizana na Fiston raia wa Burundi kwa dili la miezi sita.

Tambwe ambaye amewahi kucheza kwenye timu zote zenye maskani ya pale Kariakoo Simba na Yanga amesema kuwa ikiwa ataweza kutibu yale makosa ya timu hiyo basi atafanya makubwa ndani ya kikosi hicho kinachowania ubingwa wa ligi.

"Kusajiliwa kwa Fiston ndani ya Yanga kunakwenda kuzalisha mabao mengi ndani ya kikosi hicho kwa kuwa walikuwa wanakosa mtu wa kutengeneza na kumalizia mipango.

"Kwa namna ambavyo ninamfahamu ninajua kwamba atafanya mengi makubwa ambayo yatawapa mafanikio mabosi wa Yanga pamoja na mashabiki.

"Ni suala la kusubiri namna ambavyo atakwenda kufanya kazi na kuweza kujibu kwenye mfumo mpya wa timu yake ambayo anakwenda ila kwa upande wa kucheka na nyavu hilo analijua na anaweza kuwa msaada ndani ya kikosi hicho," amesema.

Fiston ameibukia ndani ya Klabu ya Yanga akitoka kucheza ndani ya Klabu ya ENPPI ya Misri.



Yanga ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya kucheza jumla ya mechi 18 na imefunga mabao 29.

3 COMMENTS:

  1. Miezi 6...
    Najua majiran wataanza kumtongozašŸ˜

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ila msimroge, ndo kazi yake na yuko huru kuamua acheze wapi

      Delete
  2. Hata kwa Sarpong alisema, ss hv anapigiwa hesabu za kuachwa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic